June 8, 2021

 


KADIMA Kabangu, mshambuliaji wa timu ya taifa ya DR Congo na Klabu ya Motema Pembe amesema kuwa yupo tayari kujiunga na Klabu ya Simba.

Kadima ndani ya Ligi Kuu ya Congo amefanikiwa kutupia mabao 9 katika michezo 16 na ametupia mabao matatu katika Kombe la Shirikisho barani Afrika msimu huu.

Nyota huyo amesema kuwa hana mkataba na klabu yake hivyo yupo tayari kujiunga na Simba baada ya kuwasiliana na Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes.

"Kwa sasa ndani ya kikosi cha Motema Pembe ni mchezaji huru, sina mkataba nao nipo kwenye taratibu za kujiunga na Simba.

"Taratibu hizo zinaendelea kama zitakamilika basi nitakuwa sehemu ya kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao.

"Kocha Gomes mwenyewe ndiye kila kitu kwenye suala la usajili wangu, yeye ndiye alinitafuta kisha tukawasiliana hivyo nasubiri kuona nini kitatokea mbeleni lakini Gomes ameniambia kuwa nipo kwenye mpango wake," amesema.

Kwa sasa Simba ipo kwenye hesabu za kuboresha kikosi hasa katika safu ya ushambuliaji kwa ajili ya kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa itaweza kutwaa taji la Ligi Kuu Bara.

Msimu huu imeweza kupeperusha bendera vema na kuishia hatua ya robo fainali katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic