KOCHA Mkuu wa Lazio, Maurizio Sarri amesema kuwa anahitaji saini ya kipa wa Chelsea, Kepa Arrizabalaga kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.
Sarri anataka kuongeza nguvu katika kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Anataka kumpata mchezaji huyo kwa mkopo kipa huyo namba mbili wa Chelsea ili kumpa changamoto kipa namba moja wa Lazio ambaye alicheza ndani ya Liverpool, Pepe Reina.
Kepa alijiunga na Chelsea mwaka 2018 kwa dili la pauni milioni 17 amekuwa chaguo namba mbili huku namba moja akiwa ni Edouard Mendy ambaye amejiunga darajani msimu huu.
milion 71 imekuwa 17 duh
ReplyDelete