June 16, 2021

 


KIUNGO wa Yanga, Mukoko Tonombe, amemuhakikishia Kocha Msaidizi wa AS Vita ya DR Congo, Raoul Shungu kuwa ataendelea kuitumikia Yanga kutokana na timu hiyo kumpatia huduma bora zinazomfanya atimize majukumu yake ipasavyo.

 

Mukoko amekuwa kwenye kiwango bora tangu ajiunge na timu hiyo msimu huu akitokea AS Vita, huku akifanikiwa kuitwa mara mbili kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya DR Congo.

 

Mara kadhaa Mukoko amekuwa akihusishwa kuondoka Yanga, huku timu kadhaa zikitajwa kumuwania ikiwemo Simba.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Shungu amefunguka kuwa, amezungumza na kiungo huyo na kumuhakikishia kwamba ataendelea kubaki Yanga.

 

“Ukweli nimekuwa nikiongea na Mukoko mara nyingi na amekuwa akiniambia mambo makubwa ambayo mwenyewe anasema hategemei kuondoka Yanga kwa kuwa imekuwa ikiwapa huduma bora na kuwajali wachezaji wake kitu ambacho kimechangia kiwango chake kuwa cha juu katika Ligi ya Tanzania.

 

“Lakini siyo yeye peke yake, hata Tuisila (Kisinda), kifupi imekuwa hivyo, wamekuwa na kawaida ya kuongea na mimi juu ya Yanga na ingekuwa kuna mambo mabaya wangenieleza,” alisema Shungu.

4 COMMENTS:

  1. Simba hatutaku galasa mnajitungia tu

    ReplyDelete
  2. Kwani AS Vita siku hizi ndio wasemaji na viongozi yanga?

    ReplyDelete
  3. Hebu tutazame pindi wakenda Simba, watachukuwa badala ya wacgezaji gani hata wao wawe bora kuliko ya wale waliokuwepo Simba leo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic