June 9, 2021

 


RAPA, mwanamuziki, mwimbaji na mwandishi wa mashairi kutoka Nigeria, anayerejea akitokea Uingereza, Kida Kudz, ameshusha mzigo wa nguvu ‘Ball Till We Fall’ ikiwa ni maelekezo maalum kutoka kwa Bella Smhurda, kama chaguo la muziki wa dansi ya usiku.

Staili hiyo ya muziki ni kiashiria cha kufanya kazi kwa bidii bila hofu huku ukiweka matumani posipo kukata tamaa.

Kibao hicho kipya kinaonyesha nguvu yake katika uimbaji kama msanii wa kujitegemea alipotoa kazi kali ‘Animalistic’mwaka 2001, kupitia mdundo wa ‘AFRO JIGGY’ uliopigwa tafu na Highsnobiety, Complex, Dummy, Notion, CLASH, DJ Target na wengine wengi.

 

Kazi hiyo mpya ya Kida “Ball Till We Fall” imekuja ikiwa ni tangazo la kuachia ‘sophomore mixtape’ ya TOP MEMBA ambayo itaachiliwa hewani Julai 9, mwaka huu.


Akizungumzia kibao hicho, Kida anasema: “Siku zote nilikuwa kwenye muziki wa Bella Shmurda … niliwahi kuweka kwenye ukuta wangu wa Twitter mashairi yake…. ilinifanya nimwambie kuwa tunaweza kutengeneza ngoma kali ya pamoja. Inapotokea nikawa katika muunganiko wa kazi na mtu, kabla  ya urafiki au chochote, huwa napenda kufanya muziki, hicho ni kitu kikubwa sana.

 

“Ilinichukua muda mrefu kutuma sauti yangu kwa sababu huwa napenda kufanya muziki mzuri, wenye hadhi ambao hautashusha heshima yangu kwa mashabiki. Wimbo huo kwa kweli unatuondoka kwenye mfumo wa kawaida na kutupeleka kwenye kufanya kazi kwa bidii, ubunifu, bila kukata tamaa, maadamu nguvu unazo.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic