June 25, 2021

UONGOZI wa klabu ya soka ya Azam umetamba kuwa tayari kwa mchezo wao wa nusu fainali ya kombe la Shirikisho dhidi ya Simba utakaopigwa siku ya Jumamosi, hasa kutokana na kurejea kwa mshambuliaji wao Prince Dube na kipa, Mathias Kigonya waliokuwa na majeraha. 

Dube alikosekana katika michezo miwili iliyoipita ya Azam kutokana na kuwa na matatizo ya tumbo, huku Kigonya yeye akipata majeraha hayo kwenye mchezo uliopita dhidi ya Namungo na kushindwa kumaliza mchezo.

Azam na Simba zinatarajiwa kukutana kesho Jumamosi katika mchezo wa nusu fainali ya Shirikisho, huku kumbukumbu ya mwisho kwao kukutana ikiwa ni sare ya mabao 2-2 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Februari 7, mwaka huu.

Akizungumzia maandalizi yao, Mkuu wa kitengo cha habari wa klabu ya Azam, Zakaria Thabith 'Zaka Zakazi' amesema: “Tumejiandaa vizuri kuelekea mchezo wetu wa nusu fainali na Simba tukiwa na imani kubwa ya kufanya vizuri na kufika hatua ya fainali.

“Kuelekea mchezo huo tunatarajia kuwa na nyota wetu wote wakiwemo Kigonya na Dube ambao walikuwa na majeraha, lakini tayari wamepona na wapo tayari kupambana.”

 

 

 

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic