June 25, 2021

KUFUATIA kuwepo kwa taarifa kuwa tayari beki wao wa kushoto David Bryson amemwaga wino ndani ya klabu ya Yanga, Uongozi wa klabu ya KMC, umeweka wazi kuwa haujapokea taarifa rasmi kutoka kwa mchezaji huyo, wala Yanga na wapo kwenye mpango wa kumpa mkataba mpya nyota huyo.

Bryson amekuwa na wakati mzuri akiwa na kikosi cha KMC msimu huu kiasi cha kuitwa mara kwa mara kwenye kikosi cha Taifa Stars, na kiwango chake kuzivutia timu nyingi ambazo zimeonyesha nia ya kumsajili.

Mkataba wa Bryson na KMC unatarajia kumalizika mwishoni mwa msimu huu, na taarifa zinasema tayari Yanga imempa mkataba beki huyo.

Akizungumzia taarifa hizo, Ofisa habari wa klabu ya KMC, Christina Mwagala amesema: “Ni kweli tumesikia taarifa mbalimbali zinazomuhusisha beki wetu Bryson kutakiwa na klabu ya Yanga, lakini niweke wazi kuwa hatuna taarifa rasmi kutoka kwa mchezaji husika, wala Uongozi wa Yanga kuhusiana na suala hilo.

“KMC inajitahidi kuwabakisha kwa kuwapa mikataba mipya wachezaji wetu wote ambao wamekuwa na mchango mkubwa msimu huu, lakini kama Yanga wanamuhitaji wanaweza wakampata kwa kufuata taratibu stahiki.”

5 COMMENTS:

  1. Si tulikubaliana hatuchukui free agents, bali tunachukua wa kuvunja mikataba tu?

    ReplyDelete
  2. Hao KMc Kama amekataa extension ya Mkataba na Ni anafaa asichukuliwe

    ReplyDelete
  3. Replies
    1. Ndio maana wanashinda nyuma nyuma.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic