IMEELEZWA kuwa kipa namba tatu wa Klabu ya Yanga, Ramadhan Kabwili amesepa kambini baada ya kunyimwa mkataba mpya wa kuitumikia timu hiyo.
Kabwili ni miongoni mwa wachezaji ambao mikataba yao inatarajiwa kumeguka hivi karibuni ambapo msimu huu ukiisha naye anakuwa amemaliza kandarasi yake.
Kwa mujibu wa taarifa zimeeleza kuwa nyota huyo hayupo kambini kijiji Kigamboni, Avic Town na alisepa bila taarifa kwa viongozi.
Mtoa taarifa huyo alieleza kuwa kipa huyo alikuwa anadai mkataba mpya na dau ambalo alikuwa anahitaji ni kubwa jambo ambalo mabosi wake waligomea.
"Ni ngumu kumpa mkataba mpya na fedha za usajili Kabwili kwa kuwa ni kipa namba tatu na amecheza mechi moja pekee msimu uliopita kwenye ligi.
"Msimu huu hajacheza mchezo hata mmoja kwenye ligi zaidi ya kuishia jukwaani hivyo kuongezewa mkataba na kulipwa mkwanja mrefu hayo ni matumizi mabaya ya fedha jambo ambalo ameliamua kusepa na mabegi yake kambini," .
Chanzo: Championi
Wamlipe hela zake alizocheza maiigizo ua kuhongwa na simba ili aifungishe yanga ilinhali hakuwa hata golini
ReplyDeleteKwa hiyo Yanga itabidi icheze mechi zilizobaki, ikiwamo ya Simba ikiwa na kipa mmoja tu (Farok Shikalo) maana Metacha Mnata alishasepa zake mazima
ReplyDeleteMnata alisepa kwenda wapi
ReplyDelete