June 3, 2021


 MARA baada ya kikosi chake kuingia kambini, Kocha Mkuu wa Yanga raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi ameomba michezo mitatu ya kirafiki kabla ya kurejea katika Ligi Kuu Bara na Kombe la FA.

 

Timu hiyo tayari imeanza mazoezi kwenye Uwanja wa Avic Town, Kigamboni jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa Juni 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Michezo ya ligi na Kombe la FA, hivi sasa imesimama ili kupisha kambi ya timu ya taifa, Taifa Stars inayojiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi utakaopigwa Juni 5, mwaka huu.


 Meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh amesema kuwa kocha huyo ameomba michezo hiyo kwa ajili ya kutengeneza fitinesi ya wachezaji wake.


Saleh amesema kuwa, muda wowote huenda wakatangaza timu watakazocheza nazo mara baada ya kikao cha viongozi wa benchi kukutana na kujadiliana.

 

Aliongeza kuwa kati ya timu ambazo watakazocheza nazo ipo yao ya vijana U20 itakayochezwa kwenye Uwanja wa Avic Town na lengo kocha kupata nafasi ya kuiona timu ya vijana.

 

“Ngumu kwa timu kukaa wiki mbili bila kucheza mechi za kirafiki wakati tukiwa katika mashindano, hivyo wakati muda huu ligi imesimama kocha amependekeza tucheze michezo ya kirafiki.

 

"Lengo ni kutengeneza fitinesi na utimamu wa mwili ili ligi itakapoanza, basi wachezaji wake wawe tayari kwa ajili ya mapambano.


“Zipo baadhi ya timu ambazo tutacheza nazo michezo ya kirafiki lakini kwa kuanza huenda tukacheza na timu yetu ya vijana ya U20 hapa kwenye Uwanja wa Avic Town,” amesema Saleh.


Tayari mchezo wa kwanza umeshawekwa wazi ambao ni dhidi ya African Lyon unaotarajiwa kuchezwa Juni 6,2021, Uwanja wa Azam Complex.

2 COMMENTS:

  1. Sasa mkicheza na hiyo U20 na African Lyon ndio mmeshajitayariaha,vya kutosha kwa kuchukuwa ubingwa na konbe LA Azam?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wanajiandaa kwa mechi za ligi kuu na Kombe la FA

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic