June 4, 2021

HABARI ndiyo hiyo unaambiwa, ili Yanga iweze kumsajili tena aliyekuwa mshambuliaji wao tegemezi, Heriter Makambo inatakiwa  kulipa kiasi kisichopungua milioni 100 ili iweze kuvunja mkataba wa mwaka mmoja aliobakisha na klabu yake ya Horoya.

Makambo tangia asajiliwe na klabu ya Horoya mwishoni mwa msimu wa mwaka 2018/19 akitokea Yanga ameshindwa kutamba ndani ya klabu hiyo, kiasi cha Horoya kufikiria kumuuza mchezaji huyo katika dirisha hili linalotarajiwa kufunguliwa hivi karibuni.

Taarifa za kuaminika kutoka Yanga kimethibitisha kuwa, ni kweli wapo katika taratibu za kumrejesha mchezaji huyo ndani ya Yanga ambapo tayari wameshawasiliana na klabu ya Horoya juu ya kumrudisha mchezaji huyo, ambapo wameambiwa na uongozi wa klabu hiyo wanatakiwa kulipa kiasi tajwa cha pesa ili kumrudisha mshambuliaji huyo.

“Tayari tumewasiliana na uongozi wa Horoya juu ya kumrudisha Makambo ndani ya Yanga lakini wamehitaji tuvunje mkataba wa mwaka mmoja uliobaki wa Makambo wenye thamani Dola 43,000 za kimarekani, ambazo ni sawa na  milioni 100 za kitanzania ndipo tuweze kumpata Makambo.

“Tunachoangalia kwa sasa ni namna gani tutaweza kumpata Makambo, uhakika wa kumpata upo kwa kuwa uongozi wa klabu hiyo una mipango ya kumuuza, hivyo tutafahamu mwishoni itakuwaje."

Naye Makambo kupitia mtandao wa kijamii aliandika ujumbe unaonyesha kuwa ni kweli yupo katika mpango wa kurejea ndani ya klabu hiyo ambapo ujumbe huo unasomeka: “Nimepamisi Tanzania, nimeimisi Yanga na mashabiki wa Yanga."

1 COMMENTS:

  1. Namkubali Sana makambo.kama kweli Hiyo dili Tim yngu ya yanga wats wine itakuwa POA Sana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic