June 4, 2021

 


BAADA ya Jumanne wiki hii kumsainisha mkataba wa miaka miwili mshambuliaji wao, Prince Dube Uongozi wa kikosi cha klabu ya Azam sasa uko kwenye mazungumzo na kiungo mshambuliaji wao Salum Abubakar ‘Sure Boy’ kwa ajili ya kumpa mkataba mpya.

Mkataba wa Sure Boy na Azam unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu, baada ya kiungo huyo kuhudumu ndani ya kikosi hicho kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10.

Kiungo huyo amekuwa akihusishwa na klabu mbalimbali, ambapo mwanzoni mwa msimu huu uongozi wa klabu ya Yanga ulifanya jitihada za kumsajili lakini dili hilo likayeyuka baada ya pande hizo mbili kushindwana kwenye ada ya uhamisho.

Akizungumzia mpango huo, Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Azam, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ amesema: “Baada ya kukamilisha makubaliano na mshambuliaji wetu Dube, uongozi sasa uko kwenye mazungumzo na wachezaji wetu wote ambao mikataba yao inaelekea ukingoni, ili kufanya maboresho kwenye mikataba yao na kuwapa mikataba mipya.

“Katika mchakato huu yupo pia kiungo mshambuliaji wetu Sure Boy, ambaye ni mchezaji mwandamizi na uongozi una matumaini makubwa ya kumbakisha pamoja na nyota wetu wote.”

 

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic