KYLIAN Mbappe hataondoka ndani ya kikosi cha Paris Saint Germain, (PSG) kwa namna yoyote ile kwa sasa kwa kuwa yupo kwenye mpango wa timu hiyo licha ya kuwa kwenye hesabu za kuvutwa ndani ya Real Madrid.
Nyota huyo mwenye miaka 22 mkataba wake umebakisha mwaka mmoja na yupo kwenye mpango wa mazungumzo na mabosi hao ili kuongeza dili jipya kuwatumikia PSG inayonolewa na Kocha Mkuu, Mauricio Pochettino.
Real Madrid kwa muda mrefu wamekuwa wakitajwa kuhitaji saini ya nyota huyo raia wa Ufaransa wakitajwa kuweka dau kubwa ili kumpata mshambuliaji huyo.
Kwa mujibu wa Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi amesema kuwa timu hiyo haitamuuza Mbappe na hataweza kuondoka bure ndani ya timu hiyo kwa kuwa wanahitaji huduma yake.
"Ipo wazi kwamba Kylian ataendelea kubaki ndani ya PSG. Hatuna mpango wa kumuuza kwa sasa na hataondoka bure ndani ya kikosi chetu," .
0 COMMENTS:
Post a Comment