June 7, 2021


 BAADA ya mshambuliaji wa Simba, John Bocco kufunga bao lake la 13 kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu nahodha huyo wa Simba ameweka wazi kwamba kipaumbele chake ni kuona timu hiyo ikitwaa ubingwa na siyo kupambana kuchukua kiatu cha ufungaji bora.

Kwenye ligi kwa sasa kuna ushindani mkubwa kwa upande wa ufungaji bora ambapo mtetezi wa kiatu hicho ni Meddie Kagere mwenye mabao 11.

Alitwaa kiatu hicho msimu uliopita wa 2019/20 baada ya kutupia jumla ya mabao 22 na msimu huu kinara wa mabao ni Prince Dube wa Azam FC mwenye mabao 14.

 

Bocco amesema:“Kwanza nawapongeza wachezaji wenzangu kwa kupambana na kupata matokeo mbele ya Ruvu Shooting, ulikua mchezo mgumu ambao tulitakiwa kushinda na tutaendelea kupambana mpaka tone la mwisho kwani malengo ni kunyakua ubingwa wa ligi kuu.


Kutwaa kiatu cha ufungaji bora katika ligi kuu kwangu siyo kipaumbele badala yake malengo yangu ni kuhakikisha kwamba napigana ili Simba itwae ubingwa na kama ikitokea nimefunga mabao mengi basi nitachukua hizo zawadi lakini kwa sasa malengo yangu ni kuisaidia Simba kutwaa ubingwa na sio vingine vinginevyo.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic