KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes raia wa Ufaransa, leo Juni 15 kinatarajia kukwea pipa kuelekea Moshi kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania.
Kikosi hicho kilirejea kambini rasmi Juni 8 kuendelea na mazoezi baada ya kumalizana na Ruvu Shooting, Juni 3, Uwanja wa CCM Kirumba ambapo baada ya dakika 90 ubao ulisoma Ruvu Shooting 0-3 Simba.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa umepangwa kuchezwa Juni 19, Uwanja wa Ushirika, Moshi.
Walipokutana Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Simba 2-0 Polisi Tanzania hivyo utakuwa ni mchezo wa ushindani kwa sababu Simba inahitaji kulinda rekodi na Polisi Tanzania ya Kocha Mkuu, Malale Hamsini inahitaji kulipa kisasi.
Ukitazama msimamo, Simba ipo nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 27 na pointi 67 huku Polisi Tanzania ikiwa nafasi ya 6 na pointi 41 baada ya kucheza jumla ya mechi 30.
0 COMMENTS:
Post a Comment