June 16, 2021

 


MERCEIL Ngimbi Vundi, kiungo mshambuliaji wa Klabu ya AS Maniema Union anatajwa kuwa Kwenye rada za Yanga inayonolewa  na Kocha Mkuu, Nassreddine Nabi.

Nyota huyo aliletwa duniani Aprili 18,1997 ana umri wa miaka 24 ni raia wa Congo.

Habari zimeeleza kuwa kila kitu juu ya usajili wa nyota huyo kimekamilika hivyo wapo kwenye majadiliano ya mwisho kati ya Yanga na mchezaji mwenyewe.

"Muda na wakati wowote Ngimbi atasaini mkataba wa miaka miwili wa kuicheza Klabu ya Yanga hii ni baada ya kufikia muafaka mzuri na viongozi wa Yanga.

"Tayari Ngimbi amewaambia mabosi wa Maniema kwamba anataka kwenda Yanga. Ni kati ya viungo bora sasa nchini kama usajili wake utakamilika basi watakuwa wamepata kiungo mzuri," ilieleza taarifa hiyo.

Kuhusu suala la usajili, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Injinia Hersi Said hivi karibuni alisema kuwa wamepanga kufanya usajili bora na wa kisasa.

Chanzo:Spoti Xtra

3 COMMENTS:

  1. Kwenye usajili yanga amechukua ubingwa, congo yote yake, south, zambia, ethiopia, sudan, misri , na wa ndani pia kote kazoa majembe. Msimu ujao timu zinazoshiriki vpl zijipange, utakuwa mwendo wa mkono mkono tuu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. ahahaahah washachukua ubingwa wao tayari huku kwenye VPL kupigizana kelele tu

      Delete
  2. Na muda si mrefu tutasikia wanawanyanganya Barshlona strikr wao namba moja

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic