June 5, 2021

BAADA ya kumaliza kibarua cha mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting uliopigwa juzi Alhamisi, uongozi wa kikosi cha klabu ya Simba jana (Ijumaa), uliwaruhusu mastaa wake wote walioitwa kwenye vikosi vya timu za taifa kwa ajili ya ratiba ya michezo ya Kimataifa. 

Simba ndiyo vinara wa msimamo wa Ligi Kuu ambapo mpaka sasa wamejikusanyia pointi 67, katika michezo 27 ambayo wamecheza wameshinda michezo 21, wametoa sare michezo minne na kupoteza mara mbili.

Akizungumzia hilo, Meneja wa kikosi cha klabu ya Simba, Patrick Rweyemamu amesema: “Baada ya kumaliza majukumu ya mchezo wetu wa, Alhamisi dhidi ya Ruvu Shooting, kikosi chetu kimerejea Dar es Salaam.

“Baada ya kuwasili Dar es Salaam uongozi kwa kushirikiana na benchi la ufundi, umewaruhusu wachezaji wetu wote walioitwa katika vikosi vya timu za taifa kwa ajili ya michezo yao ya kimataifa.”

 

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic