ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Ihefu amesema kuwa amewaambia wachezaji wake kuwa wana kazi kubwa ya kufanya ili kuweza kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao wa 2020/21.
Kwenye msimamo wa ligi, Ihefu ipo nafasi ya 12 ikiwa na pointi 34 baada ya kucheza mechi 30 kwa msimu wa 2020/21.
Haina uhakika wa kubaki kwenye ligi msimu ujao ikiwa itashindwa kupata matokeo katika mechi zake nne ambazo zimebaki.
Akizungumza na Saleh Jembe, Katwila amesema kuwa ushindani ndani ya ligi ni mkubwa na amewaambia wachezaji wake kwamba wana kazi ya kufanya kupata matokeo.
"Ushindani ni mkubwa na kila timu inapambana kufanya vizuri. Ninafurahi kwamba wachezaji wanaelewa na kila mmoja nimemwambia kwamba kuna kazi kubwa ya kufanya ili kupata matokeo.
"Kwa mechi ambazo zimebaki kila mmoja anahitaji kupata matokeo nasi tunahitaji kushinda hamna namna nyingine ni lazima kufanya vizuri, mashabiki waendelee kutupa sapoti," .
Tayari Mwadui FC yenye pointi 19 baada ya kucheza mechi 30 imeshuka huku ikiwa na mechi nne mkononi na msimu ujao itashiriki Ligi Daraja la Kwanza.
0 COMMENTS:
Post a Comment