June 12, 2021


 LICHA ya kuwa kwenye mpango wa kuachwa 
kwenye kikosi cha Al Ahly kutokana na kushindwa kuonyesha kiwango, mshambuliaji wa timu hiyo, Walter Bwalya raia wa DR Congo amesema kuwa bado hajawa na mpango wa kujiunga na timu yoyote nchini, ikiwemo Simba.


Bwalya amejiunga na Al Ahly mapema mwaka huu kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu akitokea Al Gouna zote zikiwa za Misri lakini ameshindwa kuonyesha kiwango katika safu ya ushambuliaji wa timu hiyo inayonolewa na Pitso Mosimane raia wa Afrika Kusini ambaye alipendekeza usajili wa mshumbualiji huyo kabla ya kuibuka kwa suala la kutakiwa kuachwa.


 Bwalya amesema kuwa mipango yake ni kuendelea kubakia kwenye timu hiyo na hana malengo yoyote ya kujiunga na klabu za Tanzania ikiwemo Simba.

"Nipo na timu ya taifa nyumbani, DR Congo, kuhusu suala na Simba au timu kutoka Tanzania, sijui chochote kwani mimi ni mchezaji wa Al Ahly na ndiyo sehemu ambayo yapo malengo yangu kwa sasa kuhakikisha timu inafanya vizuri.


"Lakini sijui kwa sasa kama nitaweza kucheza huko katika timu yoyote kwa sababu sijawa na mpango huo wala kufikiria maana nataka kuangalia malengo na mipango mingine katika sehemu ambayo nafanya kazi kwa sasa," .

7 COMMENTS:

  1. Wewe lazima uiongelee vibaya simba kwasababu upo upande wa pili.Bwalya uliongea nae lini kama siyo uongo.Jitahidi kubalance story siyo muda wote kuongelea negativity timu ya simba.Story nyingi unazitunga tu.

    ReplyDelete
  2. Kwani mtu kusema hana mpango kucheza Simba ndio negativity? Mwenzako ni mwandishi ndio maana anaandika na unamsoma! Acha kuweweseka

    ReplyDelete
  3. Sisi kama mashabiki wa nguruwe fc hatuna uwezo wa kutoa mchezaji AL AHLY, kama unabishi taja nani amewahi sajiliwa toka huko

    ReplyDelete
  4. Tunamtaka LOKOSA WETU, AMBAYE AMECHEZA MECHI NYINGI ZAIDI HAPA TANZANIA

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic