June 13, 2021


UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba bado una matumaini ya kutwaa taji la Ligi Kuu Bara lililo mikononi mwa Simba licha ya kwamba wapo nafasi ya pili.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ni mabingwa watetezi kwenye msimamo wapo nafasi ya kwanza na pointi zao ni 67 baada ya kucheza mechi 27.


Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi ipo nafasi ya pili na pointi 61 baada ya kucheza jumla ya mechi 29.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa bado hawajakata tamaa suala la ubingwa wataendelea kupambana.

"Tupo kwenye ligi na bado haijaisha jambo ambalo linatufanya tuamini kwamba bado tuna nafasi ya kutwaa ubingwa kwani kila kitu kinawezekana.

"Ushindani ni mkubwa hilo lipo wazi nasi pia tutapambana kwa mechi zetu na kupata ushindi mwisho wa siku tutajua kile ambacho tumekipata," amesema.

4 COMMENTS:

  1. Wameanza kudai point za mezani wanadhani watazipata, thubutu, wapambane uwanjani sio kukusanya mizee misangoma ndio imegeuka viongozi wa yanga

    ReplyDelete
  2. Yanga wanaume bana hawana utani na mtu, Hesabu ni kuwa wao watashinda mechi zao zote zilizobaki na Mnyama atashindwa mechi zote zilizobaki na hayo wamehakikishiwa na mganga wao aliekwisha pokea chake na kurejea kwao

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic