June 2, 2021


UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa kwa msimu wa 2020/21 Ligi Kuu Bara ilianza vizuri ila ilipoteza mvuto mwishoni.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi kwa sasa ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 61 baada ya kucheza jumla ya mechi 29 na kinara ni Simba mwenye pointi 64 baada ya kucheza mechi 26.

Ikumbukwe kwamba moja ya mchezo ambao uliyeyuka ni ule uliopaswa kuwakutanisha Simba v Yanga ambapo kutokana na kubadilishwa muda ghafla, Yanga waligomea kucheza mchezo huo kwa kueleza kuwa kanuni hazijazingatiwa.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Julai 3, Uwanja wa Mkapa baada ya ratiba kupangwa upya na Bodi ya Ligi Tanzania, (TPLB).

Hassan Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga amesema:"Ligi imepoteza mvuto hapa mwishoni kutokana na ratiba kutokuwa rafiki, yaani haijengi ile fairness katika mpira.

"Tusingeibua ile ishu kuwa kuna timu ambazo hazijacheza mechi zao sijui ingekuwaje.Kama ratiba ingekuwa nzuri zaidi tunaamini kwamba ligi ingekuwa nzuri kama ratiba itakuwa nzuri zaidi ligi itakuwa bora zaidi," .



12 COMMENTS:

  1. Huna hoja ya maana hapo,ligi imeanza vizuri kwasababu mlikua mmekalia nafasi ya watu,mnaanza kulalama kwasababu mwenye nyumba ameshaingia,poleni sana majirani zetu hii ndio simba ingawa mlitaka kuwavunja miguu.

    ReplyDelete
  2. Imepoteza mvuto kwa wasio na matumaini ya kuwa mabingwa, ila ina mvuto kwa wenye matumaini ya kuupata ubingwa. Usitusemee

    ReplyDelete
  3. Mlipokuwa mnaongoza ilikuwa na mvuto.Mlipokwama mvuto ukapotea.Hoja dhaifu isiyokuwa na mashiko.Mliahidi mnatafuta pa kutokea.

    ReplyDelete
  4. Wazee wa mapaka na madawa haooo mabingwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mkiendelea na akili zenu hizi msitegemee ubingwa miaka yote

      Delete
  5. Baiskeli ya barafu mara joto limeongezeka kidogo limeyeyuka.Visingizio vimeanza.Baiskeli ya kunolea visu kelele nyingi lakini ipo pale pale haisogei.

    ReplyDelete
  6. Chukueni majukumu ya kupanga ligi nyie basi. Hamna hoja

    ReplyDelete
  7. Ila hawa jamaa hawaoni aibu kulalamika kila siku. Hivi wangekuwa bado wanaongoza wangetamka haya? Tatizo coastal union alibutua bakuli la mboga

    ReplyDelete
  8. Watani bhana wakati mwingine mnafurahisha kwa hoja zenu zembe kabisa, ila msiwe na hofu bado viongozi wenu wana mvuto naamin pia watawavusha na kuwawezesha kubeba ubingwa wa msimu 2020/2021 kwa engineer hakuna kukwama kabisa.

    ReplyDelete
  9. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  10. majibu ya kesi ya morrison june 2 yalikuwaje kweli?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic