MSHAMBULIAJI wa Al Ahly inayonolewa na Kocha Mkuu, Pitso Mosimane raia wa Afrika Kusini huenda akasepa ndani ya kikosi hicho kwa kuwa hayupo kwenye mipango ya timu kwa msimu ujao wa 2021/21.
Kutokana na suala hilo nyota huyo amekuwa akitajwa kuibukia Simba jambo ambalo wakala wa mchezaji huyo aliweka wazi kwamba ni ngumu kwa kuwa Simba haina mkwanja wa kumpa mchezaji wake.
Nyota mwenyewe Bwalya amesema kuwa kwa sasa hajui jambo lolote kuhusiana na kuja Tanzania zaidi ya kufikiria hapo alipo ndani ya Al Ahly ya Misri.
"Sijui kuhusu kucheza Tanzania, ila ninachofikiria ni kwamba nipo hapa ndani ya Al Ahly na bado nina mipango ya kuwa katika kikosi changu hapa.
"Kikubwa ninahitaji kuipa mafanikio timu yangu pamoja na kuendelea kutimiza majukumu yangu," amesema.
Hilo ni porojo Simba si masikini wa zungusha kikapu na dunia nzima inajuwa uwezo wake
ReplyDeleteSi maskini kwa hisani ya Mo
DeleteKwan Bwalya analipwa bei gani? Inawezekana Cimba ikamlipa lkn mshahara wake huenda ni sawa au zaidi ya Gomes
ReplyDeleteyule jamaa mshahara wake anamzidi hata kocha wa simba
ReplyDeleteMSHAHARA UNATEGEMEA UCHUMI WA NCHI HUSIKA, DJUMA YANGA WATAMLIPA SHILINGI NGAPI? MILIONI 50 AU 30 AU 20? KWA MWEZI?
Delete