IMEELEZWA kuwa baada ya mabosi wa Azam FC kumpa dili la miaka miwili kiungo Charles Zulu wapo kwenye mpango wa kumtambulisha nyota mwingine tena kutoka Zambia.
Zulu raia wa Zambia yeye ni kiungo mshambuliaji tayari ameshamalizana na mabosi hao kwa dili la miaka miwili akitokea Klabu ya Cape Town City ya Afrika Kusini.
Mzambia mwingine ambaye anatajwa kuwa ndani ya ardhi ya Bongo kwa sasa ni Paul Katema ambaye naye mipango ikamilika atatambulishwa hivi karibuni.
Nyota huyo alikuwa anakipiga ndani ya kikosi cha Jeshi la Anga ya Zambia na alikuwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Zambia inayojiandaa na mashindano ya COSAFA.
Habari zimeeleza kuwa nyota huyo aliomba ruhusu kwenye timu yake ya taifa ili aje kukamilisha dili la kujiunga na Azam FC.
"Katema ikiwa ataweza kufuzu vipimo vya afya basi anaweza kusaini dili la kuitumikia Azam FC," ilieleza taarifa hiyo.
Paul Katema anachez nafasi gani?
ReplyDelete