July 20, 2021

 


UONGOZI wa klabu ya Azam umekiri kuwa kwenye mazungumzo ya kimkataba wa kuachana na mshambuliaji wao raia wa DR Congo, Mpiana Monzinzi.

Monzinzi aliyejiunga na Azam kwenye dirisha dogo la usajili ameonekana kushindwa kufikia matarajio ya waajiri wake kufuatia kuwa na mwenendo wa kusuasua, ambapo mpaka sasa ameifungia Azam mabao matatu tu. 

Nyota huyo alijiunga na Azam kama mbadala wa mshambuliaji raia wa Cameroon, Alain Thierry Akono Akono aliyeuzwa nchini Malaysia.

Akizungumzia ishu hiyo, Mkuu wa Kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Azam, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ amesema: “Ni kweli kumekuwa na mazungumzo ya pande zote mbili kati yetu na mchezaji Mpiana Monzinzi kwa ajili kuangalia juu ya uwezekano wa maamuzi yenye faida kwa pande zote mbili.

“Lakini bado mazungumzo hayo hayajafikia muafaka kwa hiyo ni suala la muda, tutatoa taarifa rasmi pale kila kitu kitakapokuwa kimepatiwa muafaka.”

 

 

 

5 COMMENTS:

  1. Nyie mnacha wakongo wakati wenzenu uto kila kukicha wanajaza wakongo

    ReplyDelete
  2. Shida we Commentor una akili ya kuabdikiwa niulize huyo Mozizi kachemka muda mbona hujapata criticism ,unapata za Sapong ,hizo Mo Energy zinawaharibu akili Wazaire waliopo Yanga mnawatukana bt wakija kwenu Ni mawakili wasomi,siyo wezi wa magari.

    ReplyDelete
  3. Ulitaka wajaze wazambia?

    ReplyDelete
  4. Na huyo Mozizi ulimpamba Sana ukitaka Yanga tuingie mkenge,lkn bahati mbaya scout ya YANGA Ni Professional na Holi litawauma,mtabakiza kuchungulia mikataba ya Wachezaji wa YANGA ikoje mmvizie labda mwende Kenya na Zambia na Uganda ndipo ujanja wenu unaishia

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic