KOCHA mkuu wa Simba, Didier Gomes amewataadharisha wapinzani wao wa jadi na wanafainali wenza wa kombe la Shirikisho Yanga kujipanga vizuri, kwani Simba inauelekea mchezo huo kwa malengo ya kulipa kisasi cha kufungwa bao 1-0 Julai 3, mwaka huu.
Simba juzi Jumapili ilikabidhiwa rasmi kombe lao la ubingwa wa nne mfululizo wa Ligi Kuu Bara katika sherehe za ubingwa zilizofanyika baada ya mchezo wao wa mwisho wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo uliochezwa kwenye uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Jumapili ijayo ya Julai 25, Simba wanatarajiwa kuwa wageni wa Yanga katika mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho utakaochezwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.
Akizungumzia maandalizi yao Gomes amesema: “Tulipoteza mchezo wa Julai 3 hapa Dar es Salaam, ni matokeo ambayo yalituumiza sana sisi pamoja na mashabiki wetu, hivyo tunakwenda Kigoma tukijua tunakwenda kwenye mchezo wa kisasi.
“Tumerekebisha makosa ambayo
tuliyafanya kwenye mchezo uliopita hasa kwenye namna ya kuanza mchezo, lakini
pia tumeongeza baadhi ya vitu na malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda ubingwa
wa FA.”
Daah utapata tabu wananch niwengi Kaka jeuli yko ilikuponza tareh 3 unarudia Tena twenzetu kigoma kwanza
ReplyDeleteSafari hii mtu atakufa kifo cha aibu sana
ReplyDelete