KOCHA mkuu wa kikosi cha Simba,
Didier Gomes amefunguka kuwa ni kweli walitarajia kukutana na mchezo mgumu
dhidi ya Yanga, lakini hakutarajia kwamba wangeweza kuwapa presha kubwa
mwanzoni mwa mchezo, hali ambayo iliwatoa mchezoni wachezaji wake.
Simba juzi Jumamosi ilipoteza
nafasi ya kutangaza ubingwa wake wa nne mfulululizo baada ya kukubali kipigo
cha bao 1-0 dhidi ya watani zao wa jadi Yanga, kwenye mchezo wa kiporo wa Ligi
Kuu Bara uliochezwa kwenye uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.
Licha ya matokeo hayo ya kipigo,
Simba imeendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara na pointi zao 73
walizokusanya katika michezo 30 waliyocheza mpaka sasa, na wanahitaji pointi
tatu kutangaza ubingwa hivyo watalazimika kujiuliza tena dhidi ya klabu ya KMC
keshokutwa Jumatano.
Akizungumzia mchezo huo, Gomes amesema: “Ni kweli nilitarajia kukutana na mchezo wa presha
kubwa kutoka kwa Yanga kwenye mchezo wetu wa Jumamosi, lakini niweke wazi kuwa
sikutarajia kama wangeweza kuanza mchezo wakiwa na presha kubwa namna ile.
“Hali hii iliwatoa mchezoni wachezaji wangu
kiasi kwamba kwa dakika 30 za kwanza ni kama vile hatukuwa uwanjani, na kwa
bahati mbaya tulikuwa tayari tumetanguliwa bao moja dhidi yao, hivyo hata
tulipokuja kurejea mchezoni japo tulijitahidi lakini tulishindwa kusawazisha
kwa kuwa walikuwa na nidhamu kubwa ya ulinzi.
“Mchezo huo umeisha na sasa tunajipanga na
mchezo wetu wa Jumatano, ambao ni wazi utakuwa muhimu kwetu kutangaza ubingwa.”
Wambie hao mashabiki zako wenyew wanafikir kufungwa na yanga eti ni uchawi
ReplyDeleteUchawi alitangaza mpili, kama ni mshabiki wa simba sawa
DeleteIMEVUJA: Julai 25 mtu anapigwa 4G
ReplyDelete