July 6, 2021

BAADA ya kufanikiwa kuibuka na ushindi muhimu wa bao 1-0 katika mchezo wao wa Jumamosi dhidi ya Simba, Uongozi wa kikosi cha klabu ya Yanga umechimba mkwara kuwa umejipanga vizuri kuhakikisha wanapata ushindi katika michezo yao miwili iliyosalia ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Ihefu na Dodoma Jiji.

Yanga juzi Jumamosi iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba katika mchezo wa kiporo wa Ligi Kuu Bara, mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam. Kutokana na matokeo hayo ya ushindi Yanga sasa imefikisha pointi 70 baada ya kucheza michezo 32 na kuzidi kujiimarisha katika nafasi ya pili ya msimamo.

Katika michezo hiyo miwili iliyosalia Yanga inatarajia kucheza nyumbani dhidi ya Ihefu Julai 14, mwaka huu na kumalizia na Dodoma Jiji ugenini Julai 18, mwaka huu.

Akizungumzia mipango yao, Ofisa habari wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli amesema: “Kwanza tunashukuru kwa kufanikiwa kuibuka na ushindi katika mchezo wetu wa kiporo dhidi ya mtani wetu Simba, na mkononi tuna michezo yetu miwili ya Ligi Kuu Bara iliyosalia.

“Mipango yetu kwa sasa ni kuhakikisha tunaendeleza moto huu kwa kushinda michezo yetu miwili iliyosalia dhidi ya Ihefu Julai 14, na baadaye Dodoma Jiji Julai 18 kwani ushindi katika michezo hii ni muhimu kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa fainali ya Shirikisho.”

 


4 COMMENTS:

  1. IMEVUJA: Julai 25 mtu anapigwa 4G

    ReplyDelete
  2. nani huyo atakaepigwa hizo 4g

    ReplyDelete
  3. Simba kutoka sare mara mbili na kufungwa mara mbili,si rahisi

    ReplyDelete
  4. Hiyo juzi mnasingizia Refa ,hizo 4g mnazokuwa mnatamba nazo kila b4 mchezo wa Yanga na hampati ,ukiacha Ile mliyosaidiwa na Tshishimbi na wale mawakala wenu waliotemwa bila kusahau ka mchezo ka Lamine Moro hata hizo Pointi msingetufikia

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic