July 20, 2021


BAADA ya msimu wa 2020/21 kumeguka na timu ya Simba kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kuna tuzo za kikosi bora ambacho hutolewa na Bodi ya Ligi Tanzania, (TPLB).


Jambo ambalo huwa wanafanya ni kutazama takwimu pamoja na mchango wa kila mchezaji kwa msimu mzima ambao ulikuwa na ushindani mkubwa.

Hapa leo ninakuletea kikosi ambacho sio rasmi kinachoweza kuunda kikosi bora kwa msimu wa 2020/21 kutokana na takwimu za wachezaji hao pamoja na mchango wao namna hii:-


Kipa ni Aishi Manula wa Simba amekuwa ni namba moja kwa makipa ambao wamekaa langoni bila kufungwa, (Clean Sheet) ikiwa ni kwenye mechi 18.

Mabeki 

 Shomari Kapombe wa Simba.

Joashi Onyango wa Simba,

 Paschal Wawa wa Simba.

Mohamed Hussein wa Simba.

Hawa ukuta wao umekuwa ni namba moja kwa ubaora ambao umeruhusu mabao 14 kwa msimu kwenye jumla ya mechi 34.


Viungo 

Mukoko Tonombe wa Yanga amekuwa ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi na ni miongoni mwa wachezaji ambao ni mhimili ndani ya kikosi hicho.

 Clatous Chama ni namba moja kwa utoaji pasi za mwisho akiwa nazo 15 ndani ya Simba na ligi kiujumla ni namba moja.

Luis Miquissone yupo zake Simba ana pasi 10 za mwisho akiwa ni namba mbili kwa wenye pasi za kutosha.



Washambuliaji

  John Bocco wa Simba ana mabao 16

 Prince Dube  wa Azam FC ana mabao 14

Chris Mugalu wa Simba ana mabao 15.


Kwako msomaji, tupangie kikosi bora cha msimu wa 2020/21

2 COMMENTS:

  1. Hapo Kikosi cha mnyama kimetajwa mara ngapi na watani mara ngapu

    ReplyDelete
  2. Ishu sio kikosi Cha Simba au Cha yanga kikubwa Ni ubora wa wachezaji

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic