UONGOZI wa klabu ya KMC umefunguka kuwa uko kwenye maandalizi mazuri ya kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mchezo wao wa kesho Jumatano dhidi ya Simba, na hawaendi kukamilisha ratiba ya kuwapa ubingwa Simba.
KMC kesho watakuwa wenyeji wa Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa katika uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.
Kuelekea mchezo huo KMC inaweza kuikosa huduma ya mchezaji wao nyota, David Bryson ambaye anasumbuliwa na majeraha ya nyama za paja.
Akizungumzia maandalizi yao, Ofisa habari wa KMC, Christina Mwagala amesema: “Tunaendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo wetu wa Ligi Kuu dhidi ya Simba utakaochezwa kesho Jumatano, ni wazi tunatarajia mchezo mgumu kwa kuwa wapinzani wetu ni timu bora, na wanatoka kupoteza mchezo muhimu wa dabi.
“Hivyo malengo yao makubwa
yatakuwa kusaka ushindi kwa namna yoyote ile, ili wajipoze na ubingwa, lakini
niwaweke wazi kuwa tumekuwa na muda mrefu wa maandalizi ya kuhakikisha tunapata
matokeo mazuri katika mchezo huu, na hatuwezi kukubali kutoa tiketi ya ubingwa
bali tutapambana kufanikisha malengo yetu.”
0 COMMENTS:
Post a Comment