July 6, 2021

 


DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba, Julai 3 alishuhudia utatu wa washambuliaji wake ukibuma kufurukuta kwa Mkapa kwa kukamilisha dk 90 bila kufunga.


Ilikuwa ni kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Yanga ambao ilikuwa ni kwa mara ya kwanza kwa Gomes kushuhudia timu yake ikimaliza dk 90 bila kufunga licha ya kuwatumia washambuliaji wake wote watatu.


Kipindi cha kwanza Gomes alianza na mshambuliaji mmoja ambaye ni John Bocco mwenye mabao 14 kipindi cha pili alimuingiza Meddie Kagere mwenye mabao 11 pamoja na Chris Mugalu mwenye mabao 10.


Mchezo huo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Gomes kutumia nyota wake wote watatu katika mchezo mmoja ndani ya ligi akiwa ameongoza mechi 15. Kwenye mechi 14 alikuwa akipenda kuwatumia washambuliaji wawili ama mmoja ila mbele ya Yanga jeshi utatu wake ulipata nafasi ya kucheza.


Gomes amesema kuwa wachezaji wake walishindwa kutumia nafasi ambazo walizipata jambo lililowafanya wakapoteza pointi tatu.


Yanga iliyo nafasi ya pili na pointi 70 ilipata bao kupitia kwa Zawad Mauya ambaye alipachika bao lake la kwanza ndani ya ligi baada ya kujiunga na Yanga.

Simba wao kwenye msimamo ni namba moja wakiwa na pointi 73 baada ya kucheza mechi 30 huku Yanga wamecheza mechi 32.

10 COMMENTS:

  1. Pia refa alichangia baada ya kuwanyima simba penati

    ReplyDelete
    Replies
    1. Penalty penalty mpaka midomo utapinda ufanane na penalty

      Delete
  2. huwezi kusikia wakiliongelea ila ikitokea kwa upande wa pili kila siku wataongea

    ReplyDelete
  3. Vipi kuhusu ile penalty ya Wawa?

    ReplyDelete
  4. VP kuhsu kad nyekundu ya boko, onyango na wawa wakimchezea kinyama tonombe

    ReplyDelete
  5. Kwani mikia fc bado tu hawakubali kuwa wamefungwa? Mkubwa ni mkubwa tu, msimu wa tatu huu kwenye ligi mkikutana na simba nyinyi ni wa kufungwa au kupata sale tena ya kusawazisha.

    ReplyDelete
  6. Kadi nyekundu ya Boko haionekani lkn penalty inaonekana,
    dah unazi mbaya sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wenzio walienda uwanjani na matokeo ya Manara mfukoni

      Delete
  7. Yanga jitahdini kucheza derby kwa mzee mpili,, cc tunakusanya makombe! Mwisho wa cku mtaacha uchawi maana mtagundua sasa mnapoteza muda kuandaa timu kishirikina kwaajili ya simba badala ya kimazoezi kuonyesha ushindani kwny ligi. Msimu wa ngap huu simba anabeba ndoo??

    ReplyDelete
  8. Kwani yale "mapaka yetu" yemeenda likizo?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic