July 29, 2021

 ULIMBOKA Mwakingwe, Kocha Mkuu wa Pamba FC ya Mwanza amesema kuwa hawadai wachezaji wake kwa kuwa walipambana mwanzo mwisho.

Ni katika mchezo wa mtoano ambapo walikuwa wakisaka nafasi ya kushiriki Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union. 

Mchezo wa kwanza Mwanza walipata sare ya kufungana mabao 2-2 ngoma ilipopigwa Tanga ikawa Coastal Union 3-1 Pamba jambo lililowafungashia virago jumlajumla Pamba.

Kocha huyo amesema:"Siwadai wachezaji wangu wamepambana kwa jasho kusaka ushindi ila mwisho wa siku bahati haijawa upande wetu.

"Mpira ni mchezo wa wazi nadhani kila mtu ameona ambacho kimetokea Tanga. Japo hatujapata nafasi lakini siwadai wachezaji. 

"Kwa hatua ambayo tumefika wanastahili pongezi nasi tunakwenda kujipanga kwa ajili ya wakati ujao,".

Pamba inapambana kurejea ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kuwa ni miaka 20 imeshayeyuka baada ya timu hiyo kushuka na kushiriki Ligi Daraja la Kwanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic