July 10, 2021

 


HAJI Omari ‘Mzee Mpili’ amezua hali ya sintofahamu, baada ya kuugua ghafla ugonjwa wa kifua.

Mzee Mpili aliugua Jumatano akiwa nyumbani kwake Ikwiriri, wilayani Rufiji, Pwani, lakini kesho yake alipata nguvu ya kufuata milioni yake aliyoahidiwa na Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara kama Yanga ikiifunga Simba.

 

Kwa muhibu wa meneja wa Mzee Mpili amesema kuwa kweli Alhamisi alichukua mzigo wake huo na kurejea zake Ikwiriri ambako inaelezwa anaendelea vizuri baada ya kupata matibabu.

 

Mzee huyo alijipatia umaarufu mkubwa katika mchezo kati ya Simba na Yanga, baada ya kudai kuwa ‘aliutengeneza’ mchezo huo kwa faida ya Yanga, na kweli wakashinda 1-0 katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Meneja wa Mzee Mpili, Mohamed Mkilalu, alisema kuwa: “Mzee amerejea Ikwiriri baada ya kwenda Dar kuchukua fedha zake kwa Haji Manara.

 

“Manara alimpa ahadi ya milioni moja endapo Yanga itaifunga Simba, kwa hiyo alimkodia usafiri wa kwenda na kurudi.


“Ni kweli alikuwa anaumwa kifua lakini sasa hivi anaendelea vizuri baada ya kutumia dozi ambazo amepewa na daktari.”

4 COMMENTS:

  1. Mungu amrejeshee siha yake iwe kama ilivokuwa kabla ya maradhi

    ReplyDelete
  2. Mungu amfanyie wepesi mzee Mpili.... Simba Nguvu Moja

    ReplyDelete
  3. Hayo majini anayobeba yatamrudi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic