July 31, 2021

 


SIMBA imeanza kwa kasi harakati zake za kusuka upya kikosi chake kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu Bara msimu ujao, baada ya kumalizana na nyota watatu fasta.

Simba imepania kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao baada ya kuishia hatua ya robo fainali msimu huu.

 

Wekundu hao wamemalizana na kipa namba moja wa Tanzania Prisons, Jeremiah Kisubi kwa kumsainisha mkataba wa miaka miwili kimyakimya.Prisons inayomilikiwa na Jeshi la Magereza, juzi ilimsajili kipa wa Mbeya City, Haroun Mandanda baada ya kupata taarifa za Kisubi kusaini Simba.

 

Simba imepanga kukifanyia maboresho machache kikosi chao katika kuhakikisha wanafanya vema katika Ligi ya Mabingwa Afrika.Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, Simba imefanikisha usajili wa kipa huyo kwa ajili ya kumpa changamoto Aishi Manula.

 

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa Simba ilifanikisha usajili wa kipa huyo haraka mara baada ya Ligi Kuu Bara kumalizika kwa kumtoa kambini saa chache huko Mbeya na kumleta jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanikisha usajili.

 

Alisema kuwa kipa huyo ameondolewa kambini na mabosi wa Simba kwa kumtaka azime simu yake ya mkononi kwa hofu ya kusumbuliwa na Yanga waliokuwa kwenye mipango naye.

 

“Prisons wametumia akili za haraka kukamilisha usajili wa kipa wa Mbeya City, Mandanda ambaye juzi walimsainisha mkataba wa miaka miwili.

 

"Wamechukua maamuzi hayo baada ya viongozi wa Prisons kumtafuta Kisubi kwa njia ya simu ambayo ilikuwa haipatikani, lakini kutokana na mmoja wa viongozi wa timu hiyo kupata taarifa za kuondoka kambini saa chache na kuja Dar kwa ajili ya kusaini Simba,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Simba pia imedaiwa kumsajili beki wa kulia wa KMC, Israel Mwenda, kwa mkataba wa miaka mitatu.

 

Mwenda kwa sasa yupo nchini Ethiopia na kikosi cha timu ya Taifa ya U-23, ambapo Simba imemalizana naye hukohuko sambamba na straika wa Mbeya City, Kibu Daniel.

 

Chanzo chetu kutoka ndani ya Simba kimeliambia Championi Ijumaa kwamba, tayari uongozi wa Simba umefanikiwa kumalizana na nyota huyo, baada ya David Kameta ‘Duchu’, kutopata nafasi nyingi za kucheza mbele ya Kapombe.


“Kwa lugha nyepesi hadi sasa 
tayari kikosi chetu kitakuwa na mbadala sahihi wa Kapombe tofauti na mwanzo,” kilisema chanzo hicho.Pia inaelezwa kuwa tayari Simba imekamilisha usajili wa winga wa kimataifa wa Malawi, Peter Banda, ambaye anaweza kuchukua nafasi ya Luis Miquissone anayewindwa vikali na Al Ahly ya Misri.Banda, 20, kwa sasa anakipiga FC Sheriff Tiraspol inayoshiriki ligi kuu ya nchini Moldovia.

 

Chanzo kilisema uongozi wa Simba ulimtuma mmoja ya viongozi katika Bodi ya Wakurugenzi ambaye alikwenda kuinasa saini ya kiungo huyo
nchini Malawi.

 

Championi Ijumaa lilimtafuta Banda azungumzie juu ya kukamilisha usajili wake wa kujiunga na Simba ambapo alisema kuwa hawezi kusema chochote juu ya kukamilisha usajili huo ingawa aliweka wazi kuwa yupo katika mazungumzo na uongozi wa Simba.

 

“Ni kweli tupo katika mazungumzo na uongozi wa Simba kwa muda mrefu, kama kitatokea chochote nadhani kitafahamika huko mbeleni,” alisema winga huyo.


Makamu Mwenyekiti wa Bodi 
ya Wakurugenzi wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ alizungumzia usajili wa Simba akisema: “Tunaendelea vizuri na mipango yetu ya maboresho ya kikosi ikiwamo kusajili wachezaji wenye uwezo mkubwa.

 

“Kila kitu kinaenda vizuri, Wanasimba wanatakiwa kutulia na kusubiri waone kazi yetu inayofanywa na viongozi wao, baada ya kupokea ripoti ya kocha Gomes (Didier) na kufanyia kazi mapendekezo yake ikiwamo usajili wa wachezaji wenye kiwango kizuri na kuwa na kikosi imara," .

10 COMMENTS:

  1. Rti wale jamaa wanasema wanautaka ubingwa kwa miaka mingi ijayo

    ReplyDelete
  2. Hivi kweli na akili yako timamu unadiriki kutuandikia utumbo huu! Kama malengo ya ubingwa wa Aftika yatafikiwa kwa kumsainisha Mwenda na Kisubi basi hongera zao. Pili, kwa maelezo yako ni kuwa Kisubi aliwazimia simu viongozi wake why ihusishwe Yanga? Suala la Banda kwa sasa yupo Maldova, why viongozi waende kupata saini Malawi? Kweli hii ni mama mkanye mwanaaaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Malawi ndiko waliko wamiliki wa Peter Banda ambao ni Butter Bullets. Nikupe shule kidogo wewe mbumbumbu. Usajili wa unafanywa kwa kumalizana na timu inayomumiliki kwa maana Peter Banda walimalizana nae kipindi kwa dau kubwa. Nafikili ushaelewa wewe mbumbumbu

      Delete
  3. Zamu ya wapigaji wa mikia

    ReplyDelete
  4. Hivi mimi nashindwa hii hesabu, eti mpangaji asipokulipa kodi ya pango kwa miaka 4,halafu akurupuke kukulipa, utamdai na riba ya hiyo miaka 4 au ndio umeuzwa kwa hasara?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Cha kuangalia ni mkataba wenu wa upangaji ulianza lini. Kama mkataba umeanza Leo anatakiwa alipe kuanzia Leo, kama mkataba ulianza miaka minne iliyopita anatakiwa kulipa miaka minne. Kama mpangaji alikuwa anaishi kwako kindugu huku mkisubiri maandalizi ya mkataba, basi someni mkataba unataka tarehe gani. HAYA MAMBO WANAELEWA WANA SIMBA TU, WA YANGA KAMA MKATABA WA MIEZI 6 WA MORRISON ULIISHA, NA UONGOZI UKAWAAMBIA WAMEMUONGEZA MIAKA MIWILI BILA KUWAONESHA MKATABA WALA PICHA ZA KUUSAINI NA WAKAAMINI WATAELEWAJE MOVEMENT ZA SIMBA?
      UTASIKIA WANAANZISHA KESI NYINGINE OOOOH TULIMSAJILI KIBU DENIS MWEEEEEEEE

      Delete
  5. Huu ni usajili wa Saleh na wajukuu zake na wala sio usajili wa Simba

    ReplyDelete
  6. mikia wote mafala tu timu wamemsusia mhindipeke yake,halafu mnajifanya mnajuaaaaa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic