July 31, 2021


 VIONGOZI wa Yanga wamejikuta wakiwa katika njia panda mara baada ya kupatwa na kigugumizi cha kuachana au kubaki kwa mshambuliaji wao, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’.


Ntibazonkiza alijiunga na 
Yanga katika usajili wa dirisha dogo uliofanyika Januari 2021 ambapo mpaka sasa ameitumikia klabu hiyo kwa nusu msimu.

 

Chanzo cha kuaminika kutoka Yanga kimeliambia Championi Jumamosi kuwa, viongozi hao mpaka sasa wameshindwa kutoa maamuzi juu ya mchezaji huyo asalie au aachwe ambapo wanaotoka aondoke wametaja sababu ni wingi wa idadi ya wachezaji wa kimataifa ambao unahitaji kuwasajili lakini pia ishu ya majeraha ya mara kwa mara.

 

“Uongozi wa Yanga unashindwa kuamua hatima ya Saido kuwa asalie au aondolewe, kama ambavyo unamuona kuwa mchezaji huyo chini ya kocha Nasreddine Nabi ameshindwa kabisa kutamba katika kikosi cha kwanza huku mara nyingi akiwa katika wachezaji wa akiba.


“Lakini pia ishu ya majeraha ya mara kwa mara ambayo amekuwa akikumbana nayo Saido na kumfanya acheze michezo michache pia imekuwa ni sababu kubwa inayomfanya mchezaji huyo kuufanya uongozi wa kufikiria uwezekano wa kuvunja mkataba wake huku viongozi wengine wakitaka mchezaji huyo asalie,” kilisema chanzo hiko.

 

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Yanga, Dominick Albinus kuhusu hatma ya mchezaji huyo, alisema kuwa wachezaji wote wa Yanga ambao watasalia ndani ya Yanga na ambao wataondoka basi taarifa itatolewa na uongozi wa timu kama ambavyo taarifa nyingine zilitolewa.

 

“Siwezi kusema lolote kuhusu hilo kwani taarifa zote za wachezaji ambao wanasajiliwa na wale watakaoachwa zitatolewa na utaratibu maalumu wa timu kama ambavyo imetokea katika utolewaji wa taarifa zilizopita,” alisema kiongozi huyo.

10 COMMENTS:

  1. Saido mzur abaki tu atatusaidia sana huyo jamaa

    ReplyDelete
  2. Kwa nini waamue viongozi kwani kocha wetu hana maamuzi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nyie mbona a nawaambia Babra. Kwani mlitaka Manara aondoke nyie

      Delete
    2. Wapenzi wa Mikia aka vichupi FC mchokezeni Babra mwone kama hamtatimuliwa wote mrudi pale kwenye jengo lenu msimbazi mkauze vijora

      Delete
    3. Kama hamuamini muulizeni Manara kilichompata. Ili kucheza na mind zenu mmepewa kiini macho cha 20 Bilioni. Hamjui hizo 20 Bilioni ni zile zile za viingilio na gawio kutoka CAF

      Delete
    4. Mwaka huu Yanga mtaumia sana na Simba

      Delete
  3. Hehehe hilo jina la vichupi fc limewakaa vizuri mikia...hahaha

    ReplyDelete
  4. Majina yote yatapita ila amini usiamini jina UTOPLLO ni la ubatizo kabisa hili litadumu milele

    ReplyDelete
  5. Utopolo hawajiamini hata kidogo maana hata akikomenti uto mwenzao wanahisi ni Mnyama. Mtateseka sana na bado misimu kibao yaani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic