July 9, 2021


 TIMU ya Polisi Tanzania, leo Julai 9 imepata ajali wakati ikitoka kwenye mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara ambazo zinatarajiwa kuendelea Julai 14.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Polisi Tanzania, kupitia akaunti rasmi ya Instagram ya Polisi Tanzania imeeleza namna hii:-Timu yetu imepata ajali wakati ikitoka mazoezini leo. Baadhi ya wachezaji wameumia.

Tunaomba mashabiki wetu na wapenda michezo waendelee kuwa na subira na taarifa rasmi itakujia hivi punde.

Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Hassan Juma amesema kuwa kwa sasa wanashughulikia afya za wachezaji pamoja na wale ambao wameumia na taarifa rasmi zitatolewa.

4 COMMENTS:

  1. Poleni sana ila isije kuwa janjajanja ya kutengeneza mazingira ya kuahirishiwa mechi ili mchungulie mechi za wenzenu ambao mpo nao kwenye mazingira hatarishi kwenye msimamo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Duh!! Poleni sana,ni kweli ajali imetokea na ilikuwa ni ajali mbaya

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic