BEKI mpya wa kushoto wa klabu ya
Azam, Edward Charles Manyama amefunguka kuwa amejipanga kuhakikisha anapambana
kwa ajili ya kuhakikisha anakuwa sehemu ya mafanikio ya waajiri wake hao wapya.
Manyama tayari ametangazwa rasmi
kujiunga Azam akitokea ndani ya kikosi cha klabu ya Ruvu Shooting aliyohudumu
kwa muda mfupi, kutokea ndani ya kikosi cha Namungo.
Akizungumza baada ya kukamilisha
usajili wake ndani ya Azam, Manyama amesema: "Nimefurahi
kukamilisha usajili wangu wa kujiunga na klabu ya Azam, kwangu kujiunga na klabu
hii ilikuwa ni ndoto yangu.
“Nimejipanga kuhakikisha
najitolea, nitajituma kadiri ya uwezo wangu ili klabu yetu iweze kuendelea
mbele."
0 COMMENTS:
Post a Comment