IMEFICHUKA kuwa benchi la ufundi
la Simba limemrudisha Zimbabwe kiungo mshambiliaji wao, Perfect Chikwende kwa
ajili kumsaidia kupata muda mwingi zaidi wa kucheza kwenye kikosi cha timu yao
ya Taifa inayojiandaa na michuano ya COSAFA, kwa lengo la kumrudishia utimamu
wa mwili.
Chikwende alisajiliwa na Simba
katika kipindi cha dirisha dogo la usajili kutokea ndani ya kikosi cha Platinum
ya Zimbabwe, mara baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika michezo miwili ya
mtoano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba.
Tangu atue Simba Chikwende
aliyekuwa akipewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri, amekuwa akipata wakati mgumu
kuingia ndani ya kikosi cha kwanza, na kupelekea kuwepo na taarifa kuwa huwenda
Simba wakafanya maamuzi ya kuachana na kiungo huyo au kumtoa kwa mkopo mwishoni
mwa msimu huu.
Akizungumzia mpango huo kocha mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema: “Ni kweli benchi la ufundi
limeamua kumrudisha Chikwende Zimbabwe, kuungana na kikosi cha timu ya Taifa ya
nchi hiyo inayojiandaa na mashindano ya COSAFA.
“Tumefanya hivi kama sehemu ya
programu maalum ya kumpa Chikwende muda mwingi zaidi wa kucheza, na kuzidi
kuimarisha utimamu wake wa mwili, na Bila shaka kama atazingatia programu
tuliyompa basi atarejea akiwa bora zaidi.
😅😅😅😅😅
ReplyDeleteMmmmmh, tatizo la usajili ya njiani
ReplyDeleteSi alikataa majaribio uyu wakat anasajiliwa atumtak
ReplyDeleteDah hatariiiiiiiiii sana anaondoka akiwa ajafikia lengo
ReplyDeleteingawa siyo haba lakini kucheza simba kiwango bado
ReplyDeleteJunior lokoxa na MZimbabwe nao wap?
ReplyDelete