July 4, 2021

KAMATI ya Waamuzi wa Ligi Kuu Bara, imeweka wazi sababu za kurudia majina ya waamuzi waliopangwa kuchezesha mchezo wa Kariakoo dabi uliopigwa jana Jumapili  kwenye uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Orodha hiyo ambayo iliwekwa wazi na Bodi ya Ligi Kuu Bara (TPLB), ilionyesha kuwa waamuzi waliochezesha mchezo wa jana ni walewale ambao hapo awali walipangwa kuchezesha mchezo wa Mei 8, mwaka huu kabla ya mchezo huo kuahirishwa.

Akizungumzia kutokuwepo kwa mabadiliko hayo, Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi Tanzania, Soud Abdi Mohamed, amesema: “Kama Kamati tuliona hakukuwa na haja ya kubadilisha waamuzi ambao walipangwa kuchezesha mchezo uliopangwa kuchezwa Mei 8, mwaka huu kabla ya kuahirishwa kutokana na sababu zilizokuwa zimejitokeza.

“Hii ni kwa sababu tayari maandalizi ya mchezo ule yalikuwa tayari yamefanyika, na kukamilika, na tuliamini kuwa waamuzi waliokuwa wamepangwa walikuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kutimiza majukumu yao kwenye mchezo wa Jumamosi."


Orodha kamili ya maofisa waliosimamia mchezo Na. 208 wa Ligi Kuu ya Vodacom (Simba SC vs Young African SC) jana Julai 3, 2021 ni kama ifuatavyo;

Kamisaa wa mchezo – Hosseah Lugano (Lindi)

 

Mwamuzi wa kati - Emmanuel Mwandembwa (Arusha)

 

Mwamuzi msaidizi namba moja – Frank Komba (Dar)

 

Mwamuzi msaidizi namba mbili – Hamdan Saidi (Mtwara)

 

Mwamuzi wa akiba - Ramadhani Kayoko (Dar)

 

Mtathmini wa mwamuzi – Soudy Abdi (Arusha)

 

Afisa mhusika – Jacquiline Kwamwamu (Dar)

1 COMMENTS:

  1. Kwa jinsi baadhi ya waamuzi wetu wa kitz wanavyotafsiri sheria za soka bado tuna safari ndefu sana ya kuchezesha mechi za caf,itaendelea kuwa ndoto za mchana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic