July 24, 2021

 


KLABU ya Simba inaripotiwa kuwa ‘Siriaz’ na mpango wa kumsajili kiungo mshambuliaji kinda wa kimataifa wa Malawi, Peter Banda anayekipiga kwa mkopo ndani ya klabu ya Sheriff Tiraspol akitokea klabu ya Nyasa Big Bullets.

Simba inataka kumuongeza Banda mwenye umri wa miaka 20, kama mbadala wa Mzimbabwe, Perfect Chikwende ambaye ameonekana kupata wakati mgumu kuendana na utamaduni wa Simba kiasi cha kuondolewa kikosini, huku taarifa zikieleza kuwa huenda Simba ikaachana naye au kumtoa kwa mkopo mwishoni mwa msimu huu.

Hivi karibuni mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Zacharia Hanspope alifunga safari na kwenda nchini Malawi, huku ikielezwa kuwa miongoni mwa usajili wa wachezaji ambao alikuwa amekwenda kumalizana nao ni ule wa Banda.

6 COMMENTS:

  1. Mpira wa Kibongo ni mpira wa wapiga dili,Chikwende amecheza match ngapi? Mpaka useme kiwango kipo down? Angecheza match nyingi tungesema kiwaango duni,ndiyo yaliyomkuta Kagere msimu huu,hachezeshwi match nyingi then wanasema Kagere kashuka kiwango,kweli mpira wa Bongo kichefuchefu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe ni utopolo ndiyo maana unatoa very biased analysis vs Simba SC. Chikwenda hatufai!!!!

      Delete
    2. Achilia mbali ushabiki, usajili wa Chikwende ulikuwa wa kukurupuka.

      Delete
    3. HAWAKUKURUPUKA ULIKUWA USAJILI MZURI ILA MCHEZAJI AMESHINDWA KUFIKIA MALENGO AMBAYO TIMU WALITARAJIA.... LEO HII GRIEZMAN ANAONDOKA BARCELONA, KWANINI AWE GRIEZMAN NA ASIWE ANSUFAT AU MESSI MWENYEWE AONDOKE? HAPA NDIPO TUNATAKIWA KUELEWA KWAMBA KUNA WACHEZAJI WANASAJILIWA KWA MALENGO NA MATOKEO CHANYA YA HARAKA.

      Delete
  2. Kwani hujuwi kuwa viwango huamuliwa kutokana na mazowezi ya kila siku na anapopewa fursa yakucheza?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic