July 24, 2021

IMETHIBITISHWA kuwa Uongozi wa klabu ya Yanga upo kwenye mazungumzo na kiungo wa Kimataifa wa kimataifa wa Ghana anayecheza soka la kulipwa kwenye klabu ya Cleopatra inayoshiriki Ligi Kuu nchini Misri, Kwame Bonsu ili kuimsajili kwa ajili ya msimu ujao wa 2021/22.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya kikosi cha klabu ya Yanga kimesema kuwa, tayari mabosi wa klabu hiyo wamekubali kulieweka jina la kiungo huyo wa Ghana ambaye amesaliwa na mwaka mmoja tu kwenye mkataba wake wa katika listi ya nyota wapya wanaotarajiwa kusajiliwa kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

“Ni kweli Uongozi kwa kupitia Kamati yetu ya usajili umekubaliana na maamuzi ya kujumuisha jina la kiungo wa Ghana, Kwame Bonsu kwenye listi ya nyota wapya ambao wanatarajiwa kusajiliwa kwa msimu ujao.

“Hii ni baada ya kumfuatilia na kugundua kuwa ni miongoni mwa viungo bora Afrika, lakini pia ni kiungo mwenye uzoefu mkubwa na michuano mikubwa akiwa tayari ameshacheza kwenye timu kubwa kama Esperance ya Tunisia na Asante Kotoko ya Ghana.”

Akizungumzia kuhusu usajili wa kiungo huyo Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano wa klabu ya Yanga, Thabit Kandoro amesema: “Kwa sasa tumesitisha kwa muda kujihusisha na masuala ya usajili, kwa kuwa bado tuna kibarua cha mchezo wetu wa fainali ya kombe la FA dhidi ya Simba Julai 25, mwaka huu na tutazungumzia masuala ya usajili baada ya mchezo huo kukamilika.”

 

 

2 COMMENTS:

  1. Kwenye usajili tuizoea mikwara yao..subiri ligi ianze ndo utajua kwann hawa watu ni utopolo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic