July 18, 2021


 KLABU ya Simba leo Julai 18 imekabidhiwa taji la Ligi Kuu Bara baada ya kukamilisha mzunguko wa pili kwa msimu wa 2020/21.

Mchezo wa leo Uwanja wa Mkapa ubao umesoma Simba 4-0 Namungo na kuifanya timu hiyo kufikisha jumla ya Pointi 83.

Namungo inabaki na pointi zake 43 na msimu huu wa 2020/21 imekwama kupata pointi hata moja mbele ya Simba.


Mchezo wa kwanza Uwanja wa Majaliwa ubao ulisoma Namungo 1-3 Simba na kufanya timu hiyo kuyeyusha jumla ya pointi sita mazima.

Mabingwa hao wa ligi wamefanikiwa kutwaa taji hilo mara nne mfulilizo ambapo Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa sababu ya kufanya hivyo ni uwekezaji mzuri.

"Uwekezaji mzuri kwa wachezaji pamoja na sapoti ambayo tunapata kutoka kwa mashabiki ni nguvu kwetu kuona kwamba tunashinda mechi ambazo tunacheza.

"Hakuna namna shukrani kwa mashabiki kwa jambo hili na tunaamini kwamba msimu ujao utakuwa wa tofauti zaidi," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic