TIMU nne kwa sasa zinatarajiwa kutangazwa rasmi na Bodi ya Ligi Tanzania, (TPLB) kwamba msimu ujao zinaweza kushiriki Ligi Daraja la Kwanza.
Kwa namna ambavyo msimamo wa Ligi Kuu Bara upo ni timu nne zipo kwenye mstari mwekundu ambao unaonyesha kwamba timu hizo zitashuka daraja na msimu ujao wa 2021/22 zitashiriki Ligi Daraja la Kwanza.
Timu hizo ni pamoja na:- JKT Tanzania ikiwa nafasi ya 15 na pointi zake ni 39, Gwambina FC ambayo imemaliza ikiwa nafasi ya 16 na pointi zake ni 35.
Pia ipo Ihefu FC ina pointi 35 nafasi ya 18 na Mwadui FC nafasi ya 18 na pointi zake ni 19.
Pia mbili zipo kwenye nafasi ya kucheza hatua ya mtoano ambazo ni pamoja na Mtibwa Sugar iliyomaliza msimu ikiwa nafasi ya 14 na pointi 39 pamoja na Coastal Union iliyomaliza ikiwa nafasi ya 13 na pointi 40.
0 COMMENTS:
Post a Comment