WAMEPANIA ndivyo unavyoweza
kusema kufuatia Uongozi wa Azam kufuta Tamasha la Azam, huku
wakitumia muda huo kwenye maandalizi, ambapo kesho Jumatatu kikosi kitasafiri
kuelekea Zambia kwa ajili ya muendelezo wa maandalizi kabla ya msimu ‘pre-season’.
Agosti 14, mwaka huu Azam ilianza
rasmi kambi kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Wakiwa Zambia, Azam
wanatarajia kuwa na michezo minne ya kirafiki dhidi ya klabu za Red Arrows,
Forest Rangers, Zanaco pamoja na Zesco.
Akizungumzia mipango yao, Mkuu
wa Kitengo cha Habari na mawasiliano wa Azam, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’
amesema: “Baada ya kuwa na wiki moja ya mazoezi, kwenye uwanja wa Azam Complex,
kikosi chetu kitaondoka nchini Agosti 23, kuelekea Ndola Zambia kwa ajili ya
maandalizi ya wiki moja na nusu.
“Tukiwa huko tunatarajia kuwa na michezo minne ya kirafiki dhidi ya Red Arrows Agosti 25, Zanaco Agosti 29, Forest Rangers Septemba 2, na Zesco Septemba 3, mwaka huu, baada ya hapo tutarejea kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kombe la Shirikisho.
Azam Festival
“Kuhusu tamasha la Azam ambalo lilianza mwaka uliopita halitakuwepo mwaka huu, tunaomba radhi lakini
hii inatokana na ratiba ngumu ya maandalizi hivyo isingewezekana kukatisha
programu ya mwalimu kwa kuwa malengo yetu ni makubwa msimu ujao.”
Wacha mvua inyeshe tuone panapovuja...wacha ligi ianze tuone pasipoonekana.
ReplyDeleteKambi ya mwezi mmoja Simba nchini Morocco itawarahishia kuwaunganisha zaidi kitimu. Naona Yanga wanatumia muda mwingi zaidi kuimarisha pumzi zao ila nadhani wanahitaji muunganiko zaidi.
Nawatakia mandalizi mema timu yangu ya Azam fc
ReplyDeleteSimba miamba kwa kipindi/Karne wanatumia akili Sana,,,
ReplyDelete