August 22, 2021


HAKUNA kisingizio Septemba 25 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii ambao utakuwa ni ufunguo wa msimu mpya wa Ligi Kuu Bara 2021-22, Simba na Yanga wakishuka dimbani.

Utamu wa mchezo unazidi kuongezeka kutokana na vikosi vyote viwili kuonekekana kuimarika zaidi kutokana na usajili ambao umefanywa hadi sasa kwa kila upande.

Yanga waliteswa sana na eneo la ushambuliaji msimu uliopita, na ndiyo maana kwenye dirisha hili la usajili wamecheza zaidi kwenye eneo hilo kwa kusajili nyota ambao wanaamini wataleta mabadiliko.

Kwa usajili wa timu zote ambao umefanyika hadi sasa, Yanga wanaonekana kuimarika zaidi kwenye eneo la mbele wakiwa na maingizo mapya, Fiston Mayele, Heritier Makambo, Jesus Moloko na Dickson Ambundo.

Ambao wanakwenda kuungana na nyota kama Deus Kaseke, Ditram Nchimbi na Yacouba Sogne.

Wakati Yanga wakitamba na washambuliaji zaidi, Simba wao hawakuwa na shida sana kwenye eneo hilo baada ya kuwepo nyota kama John Bocco, Chris Mugalu na Meddie Kagere.

Wao wakaamua kucheza na viungo zaidi, wakimleta Peter Banda, Duncan Nyoni, Ousmene Sakho, Abdulswamad Kassim,na Sadio Kanoute ambao wanakwenda kuungana na Tadeo Lwanga, Jonas Mkude, Said Ndemla, Hassan Dilunga na Raly Bwalya.

Hata hivyo ukiachana na timu zote kutamba na usajili wao huo msimu huu,timu hizo hadi sasa kutokana na sajili walizozifanya wamefanikiwa kutengeza vikosi viwili hatari yaani kikosi cha kwanza na cha pili, vyote kuonekana kuwa hatari.

Kwa upande wa Yanga wao kikosi chao cha kwanza chini ya kocha Nadreddine Nabi kinatarajiwa kuwa hivi 1.Diarra Djigui 2.Djuma Shabani 3.David Bryson, 4.Bangala Litombo 5.Bakari Mwamnyeto 6.Mukoko Tonombe 7.Feisal Salum, 8.Khalid Aucho, 9.Heriter Makambo, 10.Fiston Mayele, 11.Yacouba Songne

Kikosi cha pili cha Yanga kinatarajiwa kuwa na nyota hawa kipa 1.Erick Johora 2.Kibwana Shomari, 3.Yasin Mustapha 4. Abdallah Shaibu Ninja, 5.Dickson Job, 6.Zawadi Mauya, 7.Ducapel Moloko, 8.Deus Kaseke, 9.Yusuph Athumani, 10.Saido Ntibazonkiza, 11.Dickson Ambundo.

Watakaosubiri ni Ramadhani Kabwili, Adeyum Salehe, Balama Mapinduzi, Paul Godfrey Boxer, Farid Mussa na Ditram Nchimbi.

Kwa upande wa Simba wao kikosi chao cha kwanza kinatarajiwa kuwa hivi 1.Aishi Manula, 2.Shomari Kapombe, 3.Mohammed Hussein Tshabalala, 4.Henock Baka, 5.Joash Onyango, 6.Taddeo Lwanga, 7.Peter Banda, 8.Rally Bwalya, 9.Chris Mugalu, 10.John Bocco, 11.Pape Ousmane Sakho.

Kwa upande wa kikosi cha pili cha Simba chenyewe kinatarajiwa kuwa hivi 1.Beno Kakolanya, 2.Isra Mwenda3. Gadiel Michael, 4.Erasto Nyoni, 5.Henock Baka, 6.Jonas Mkude, 7.Bernard Morrison, 8.Sadio Kanoute, 9.Meddie Kagere 10.Yusuph Mhilu 11.Duncun Nyoni.

Wanaobaki katika kikosi cha Simba watakuwa ni Jeremia Kisubi,Perfect Chikwende,Hassan Dilunga,Said Ndemla,Abdulswamad Kassim,Mzamiru Yassin,Ibrahim Ame,Kibu Denis.

 

 

 

 

2 COMMENTS:

  1. Jimmyson Mwanuke aliyesajiliwa juzi juzi tu atatolewa mkopo?????

    ReplyDelete
  2. Mwinuke hatolewi kwa mkopo umri sio sababu ya mchezaji kutolewa kwa mkopo. Mwinuke ni kijana mwenye kipaji maalum licha ta umri wake kuwa Mdogo akikaza atatoboa mapema tu wanaomsimia wanatakiwa kumtafutia daftari la Mbwa samata ndani ya Simba.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic