August 3, 2021


 UONGOZI wa Kagera Sugar Football Club unapenda kutoa taarifa kwa wanamichezo pamoja na Wanahabari kuwa umeamua kutowaongeza mikataba mipya wachezaji 8 ambao mikataba yao imetamatika mwisho wa msimu wa 2020/2021.

Taarifa rasmi iliyotolewa Agosti 3 na Kagera Sugar ipo namna hii:-

Wachezaji hao wote hawatokuwa sehemu ya kikosi kiatakacho ingia kambini katika maandalizi ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania bara 2021/2022 ambayo inatarajia kuanza muda si mrefu.


Wachezaji hao ni Pamoja na:
Benedict Tinocco (mlinda mlango), Haroun Mussa (Beki),Hassan Isihaka (Beki), Ali Sonso(Beki), Mohammed Ibrahim (Kiungo), Mussa Mossi(Kiungo).

 Abdulswamadu Kasim (Kiungo),Vitalis Mayanga(Mshambuliaji).

Makubaliano hayo yamefanyika baina ya benchi la ufundi,wachezaji pamoja na uongozi na kufikia muafaka wa kuwaruhusu waende kutafuta changamoto sehemu nyingine ili waweze kuendeleza mapambano. 

Uongozi unapenda kuwashukuru kwa michango yao mikubwa walioionesha kuipambania timu kwa kujitoa kwa hali na mali tangu siku ya kwanza ambapo waliamua kuwa wanafamilia ya Kagera Sugar hadi leo tunafikia tamati.

Mazuri yenu tutayaenzi na kuyakumbuka daima na hakika mmetuachia maswali magumu sana mioyoni mwetu lakini waswahili wanasema 'Hakuna lenye mwanzo lisilokuwa na mwisho'.

Tunawatakia kila la Kheri katika changamoto zetu mpya mtakazoenda kukutana nazo katika tasnia hii ya mpira wa Miguu na Mungu awaongoze katika kila hatua mtakayokuwa mnaiendea katika mapambano mapya.

3 COMMENTS:

  1. Halafu nyie jamaa wa kiblog hiki mkaja na habari zenu za kutunga kuwa eti Abdulswamadu Kassim anatakiwa Simba ilhali hata huko Kagera hawana haja nae kutokana na kiwango duni,angalieni aina ya wachezaji wa kuwadalalia

    ReplyDelete
  2. Yn mo ibrahim ht kagera wamemtema??? Dah! Wachezaj wetu wa bongo wana shda sn,, kwann hawadumu???

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic