September 9, 2021

 


UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Horseed FC ya Somalia yanaendelea na jana waliweza kufanya mazoezi rasmi wakiwa wachezaji wote.

Hii ni baada ya wachezaji wengine kuwa nje ya kambi ya Azam FC iliyowekwa Zambia kutokana na kuwa na majukumu kwenye timu zao za taifa.

Miongoni mwa wachezaji hao ni Idd Seleman, 'Nado' Sure Boy na Mudhathir Yahya ambao walikuwa kwenye timu ya taifa ya Tanzania ambayo iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Madagascar kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa kila kitu kinakwenda sawa kwa kuwa wachezaji wanahitaji kufanya vizuri. 

"Mazoezi yanakwenda vizuri na jana wachezaji waliweza kucheza wote kwa pamoja baada ya wengine kuwa kwenye majukumu yao ya timu ya taifa na hatukuwa nao kambini Zambia.

'Maelekezo ambayo tumepewa ni kwamba hakutakuwa na mashabiki na wale ambao wataingia wanapaswa kupima Corona wale wote watakaoingia," amesema.

Mchezo huo wa Kombe la Shirikisho hatua ya awali unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex,  Septemba 11 saa 1:00 usiku.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic