September 9, 2021


 UONGOZI wa Mtibwa Sugar umeweka wazi kuwa unahitaji kufanya makubwa kwa msimu mpya wa 2021/22.


Kwa misimu miwili mfululizo,  Mtibwa Sugar imekuwa katika mwendo wa kusuasua na uliweka wazi kuwa msimu wa 2019/20 ni moja ya msimu mbovu kwao.


Msimu wa 2020/21 ilinusurika kushuka daraja baada ya kushinda kwenye mchezo wa play off dhidi ya Transit Camp ambayo inashiriki Ligi Daraja la Kwanza ambayo kwa sasa inaitwa Championship. 


Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa wapo imara na wanaamini watakuwa tofauti kwa msimu mpya.


"Tupo imara na tutafanya mengi mazuri kwa ajili ya mashabiki ambao wanahitaji kuona mambo mazuri, kikubwa wazidi kuwa nasi bega kwa bega,".


Mtibwa Sugar ina maingizo mapya ikiwa ni pamoja na nyota kutoka TS Galaxy inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini ambaye ni Abdi Banda pia ina saini ya nyota Said Ndemla ambaye ni kiungo mshambuliaji kutoka Simba.

1 COMMENTS:

  1. Wachezaj bongo wakipata dili nje huwa awadumu,,, km huyu banda cjui n nn kilimpata! Ht timu ya taifa km c mara moja tu aliitwa bac n mara 2 tuu tofaut na alpokuwa bongo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic