September 19, 2021


WAKIWA nchini Nigeria wawakilishi wa Tanzania wamepata nafasi ya kupata nasaha kutoka kwa  Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Dkt. Benson Bana.

Bana alikutana alikutana na viongozi, benchi la ufundi pamoja na wachezaji ambao wapo nchini Nigeria.

Kambi yao ipo mjini Port Harcourt, Nigeria ambapo wanamchezo wa marudio wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Rivers United ikiwa ni hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kiongozi huyo alipata muda wa kuzungumza machache pamoja na kuwapa hamasa wachezaji wa Yanga kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Rivers United FC.

Kwa mujibu wa nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto amesema kuwa wamekubaliana kupambana ili kupata matokeo chanya kwenye mchezo wa leo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Haji Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wapo tayari na watapambana kwa jasho jingi kupata ushindi.


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic