September 20, 2021


MCHAMBUZI wa masuala ya michezo Tanzania ambaye pia ni mchezaji tegemeo kwenye timu ya Wanahabari za Michezo Bongo Anwary Binde amesema kuwa mchezo wa jana ulikuwa ni kipimo tosha kwa Simba.

Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 kwenye tamasha la Simba Day, ubao ulisoma Simba 0-1 TP Mazembe na kuwafanya wenye shughuli yao mambo kutibuka jioni.

Ulikuwa ni mchezo wa kukata na shoka kwa kuwa dakika zote 90 ilikuwa ni kazikazi kwa timu zote mbili na mashabiki walijitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo pamoja na burudani 

 Binde amesema;"Ulikuwa ni mchezo mzuri na kipimo kwa Simba hasa kutoka kwa TP Mazembe na kwa namna takwimu ambazo zilikuwa waliweza kuwa na uwiano mzuri lakini TP Mazembe waliwazidi Simba.

"Jumla TP Mazembe walipiga pasi 511 zilifika pasi 451 na zilipotea pasi 60 kwa upande wa Simba wao walipiga jumla ya pasi 474 ni  415 zilifika na 59 zikapotea," amesema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic