September 6, 2021


HAJI Manara, Ofisa Habari wa Yanga amemtwika mzigo mzito mshambuliaji mzawa, Ditram Nchimbi kwa kumtaka afunge mabao mengi kwa msimu mpya wa 2021/22.

Manara amesema kuwa uwezo ambao anao Nchimbi ni mkubwa jambo ambalo anatakiwa kulifanya ni kushirikiana na wachezaji wenzake katika kufunga mabao na kuipa timu hiyo ubingwa wa 28 ndani ya Ligi Kuu Bara.

“Nchimbi ni mshambuliaji mzuri unaweza kumfananisha na Buffalo, (nyati) hivyo kwa msimu ujao kazi yake itakuwa ni kufunga mabao tu, Wananchi wanataka mabao,”.

Huo utakuwa ni mzigo mzito kwa Nchimbi kwa kuwa msimu wa 2020/21 katika jumla ya mechi 25 akitumia dakika 973 alifunga bao moja na kutoa pasi tatu za mabao.

Kinara wa utupiaji alikuwa ni Yacouba Songne ambaye alifunga jumla ya mabao nane ndani ya Ligi Kuu Bara na alitoa pasi sita za mabao.

2 COMMENTS:

  1. Hivi haji katangazwa lini kuwa afisa habari wa yanga? Baada ya kutua yanga sasa nchimbi amekuwa mchezaji mzuri?

    ReplyDelete
  2. Wow, happy to see this awesome post. I hope this think help any newbie for their awesome work. By the way thanks for share this awesomeness from play free slots online

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic