September 10, 2021


 HAJI Manara, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa timu yenye makombe mengi ndani ya Tanzania ni Yanga na hao ni mabingwa wa muda wote.

Awali alipokuwa ndani ya Simba kabla ya kubwaga manyanga aliwahi kuweka wazi kuwa timu hiyo ya Simba ilikuwa ni namba moja kwa kutwaa mataji mengi ila kwa wakati huu anasema kuwa Yanga ni mabingwa mara nyingi.

Manara ameweka wazi kuwa huwezi kusema kuwa Simba amechukua Kombe ubingwa mara sita wakati Yanga amechukua mara tano wakati kuna data nyingine ambazo hazijawekwa.

"Mabingwa wa muda wote ndani ya Tanzania ni Yanga, hizo namba zote ambazo unaziona nilizitengeneza mwenyewe, hivyo haziwezi kunitisha kabla ya kujiondoa.

"Ikiwa utaweka orodha ya mabonanza pamoja na mambo mengine basi Yanga inaweza kuwa na mataji bilioni ambayo tumeyatwaa hivyo hakuna namna kwa fact, (ukweli) sisi tunaongoza kwa kutwaa mataji mengi.

"Achana na porojo za nyuma kwa fact Yanga ina mataji mengi kuliko klabu yote Tanzania, nilifanya makosa ya kudangaya," .  

8 COMMENTS:

  1. So what? Huyu awahishwe mirembe hospital

    ReplyDelete
    Replies
    1. Manara ni mgonjwa ila watu hawajamstukia.

      Delete
    2. Nmecheka kwa sauti ujue!! Una mawazo km yangu kabisa

      Delete
  2. Kwa hiyo mataji hayo ni ya lini?

    ReplyDelete
  3. Tutajiridhisha vipi kama sasa hivi hudanganyi? Wananchi tuwe nae makini huyu mtu

    ReplyDelete
  4. YANI JINSI UNAVYOWEWESEKA NI SAWA NA KUVUA TAULO MBELE YA MKWEO TENA UKIWA UMETOKA KUOGA NA MAPOVU MASIKIONI,UNAJIDHALILISHA SANA MANARA,NINGEKUSHAURI JAMBO VITABU VYA DINI VINASEMA HEKIMA HAIPAYUKI WALA HAIONGOPI,KWANIN UNAUTUMIA ULIMI WAKO VIBAYA?JIULIZE JE UTAISHI HAPO MILELE?VIPI KUHUSU MUAJIRI WAKO MPYA BAADA YA KUONDOKA HAPO UTAMUAMINISHA VIPI KUHUSU UAMINIFU WAKO MAANA UNAONEKANA WEWE NI MROPOKAJI NA MPIGA POROJO.POLE SANA MANARA NA POLENI PIA YANGA NA HONGERA SANA SIMBA KWAKUTAMBUA KWAMBA KUNA KIRUSI NDANI YA SIMBA NA KIMETUTAFUNA KWA MUDA MREFU SANA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mpe vidonge vyake mwendawazimu huyo. Nawaonea huruma Utopolo kwa kubeba kirusi hicho hatari

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic