September 26, 2021


 JANA ulichezwa mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Simba v Yanga na mwisho wa siku mshindi aliweza kujulikana baada ya dakika 90.

Ilikuwa ni lazima mshindi apatikane kwa namna yoyote ile na mwisho wa siku ikawa kama ilivyotokea kwa timu ambayo imetumia makosa ya mpinzani.

Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 0-1 Yanga hivyo kwa sasa furaha ya mashabiki wa Yanga ipo kwenye taji lao la kwanza kwa msimu mpya wa 2021/22 ambao unatarajiwa kuanza kesho.

Hakuna namna Yanga mnastahili pongezi kwa ambacho mmekifanya na inaonyesha kwamba mlikuwa mnadhamira ya kusepa na taji na mwisho wa siku imekuwa hivyo.

Kwa Simba kupoteza mchezo ni sehemu ya mchezo na hilo lipo wazi hakuna namna maisha lazima yaendelee na pale ambapo mmefanya makosa benchi la ufundi nina amini kwamba litafanyia kazi makosa.

Imeanza kuonekana mapema lakini hili inabidi lifanyiwe kazi hasa kwenye upande wa ushambuliaji ambao katika mechi mbili Simba imeonekana ikipata tabu katika kumalizia nafasi ambazo inazitengeneza.

Ikumbuke ile mechi ya kirafiki ambapo Simba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya TP Mazembe na mwisho wa siku ilikuwa ni maumivu kwa mashabiki wa Simba.

Pia ilikuwa inaonyesha kwamba ile safu ya ushambuliaji haikuwa na makali ambayo yalikuwa yanaonekana kwenye mechi zilizopita na mwisho wa siku Simba ikashindwa kupata ushindi.

Ngoma ilikuwa ngumu pia kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii baada ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga haina maana kwamba haina uwezo basi ni makosa ambayo yanafanyika.

Ikumbukwe kwamba Simba inakazi ya kuiwakilisha Tanzania kimataifa na hapo kazi inapaswa kuwa kubwa zaidi ikiwa hakutakuwa na mipango makini basi Simba itakwama kutinga hata hatua ya robo fainali.

Kikubwa ambacho kinatakiwa kwa sasa ni kila mmoja kuweza kuangalia namna ya kuweza kuboresha makosa ambayo yamefanyika na mwisho wa siku kuacha maisha yaendelee.

Suala la kuanza kumtafuta mchawi ni nani kwa sasa muda wake umeisha jambo la msingi ni kuona kwamba kila mmoja anatimiza majukumu yake.

Kwenye Ligi ya Mabingwa ni muhimu kufanya vizuri ili kuweza kufikia malengo ambayo Simba imejiwekea kila kitu kinawezekana hivyo ni suala la kufanya maandalizi mazuri.

Wachezaji wa Simba ambao ni wapya wote ni wazuri ila tatizo kubwa lipo kwenye uzoefu wa mechi za ushindani na zile za kimataifa kwa upande wa ligi ya ndani ipo wazi ushindani utakuwa mkubwa ila kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ni muhimu kujipanga zaidi na zaidi.

Yote yanawezekana hakuna haja ya kutafuta mchawi maandalizi mazuri ni muhimu na kufanya kazi bila kukata tamaa.

Pongezi kwa Kennedy Juma, hapaswi kubweteka hasa akiwa ni mzawa ni lazima aongeze nguvu zaidi na kupambana bila kuchoka.

Hakuna namna wazawa wana nafasi kubwa ya kupeperusha bendera ya Tanzania lakini haitakuwa rahisi bila ya kujituma bila kukata tamaa.

Kilichowafanya Simba wakapoteana ni kushindwa kuwa na utulivu katika mchezo wa jana jambo ambalo liliweza kuwafanya wacheze faulo nyingi tofauti na wapinzani wao Yanga ambao walionekana kucheza kwa kujiamini.

Faulo 26 sio mchezo kwa timu aina ya Simba na namna ambavyo imekuwa ikicheza lakini ni mpira na matokeo lazima yapokelewe hakuna anayeweza kuyabadili.

Kwa kadi nyekundu hakuna namna ilikuwa lazima iwe hivyo kwa sababu Taddeo Lwanga aliweza kucheza faulo nyingi kwenye kucheza mpira na mwisho wa siku akaonyeshwa kadi mbili za njano.

Mabadiliko ya lazima hayakuwa na chaguo kwa Kocha Mkuu, Dider Gomes kwa kuwa alilazimika kuwatoa wachezaji wake ikiwa ni Joash Onyango pamoja Kanoute.


Imeandikwa na Dizo Click 

9 COMMENTS:

  1. Subiri simba atolewe kimataifa ndipo uandike ujinga wako,aliyepoteana kimataifa ni yanga na hata jana kama sio kukamia mechi hakuna lolote,mbinu zilizotumika zinajulikana,mbio ndefu yanga hawezi na kama unabisha subiri ligi ianze utaamin maneno yangu.kufungwa ni kawaida man jana kapigwa na villas acheni kukariri yangu na waandishi uchwara.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hasira za nini ng'ombe weeee... Kama unajua ni mwandishi uchwara sasa umefuata nini kwenye page yake.... MACHUPI FC.. tutawapiga sana mpaka hasira zenu ziwaishie

      Delete
    2. Hapo umeongea kiongozi mbio ndefu yanga hawawezi viini macho vyakuitengenezea simba wanabaki wanacheza hapahapa bongo hamna tena neno kimataifa tumechoka kubeba kichaa kila siku anatuchafua ngao ya jamii kashiriki kwa viti maalum

      Delete
  2. Mashabiki wa simba wengi hawajui mpira kumbe,eti yanga walipaniki kama walipaniki nadhani takwimu ya fouls nyingi zingekuwaa yanga,hilo ndo soccer asiyekubali kushindwa siyo mshindani Huyo,

    ReplyDelete
  3. Mwandishi umekosea unge wasifia simba hivyo ndivyo wanataka

    ReplyDelete
  4. Hivi akili za mikia fc ziko miguuni au matakoni? Sasa badala ya kukubali mmefungwa unaanza kumlaumu mwandishi, dah!!

    ReplyDelete
  5. Mpira Ni starehe sio Vita wala uadui tuweni wastaarabu

    ReplyDelete
  6. Always win through actions and not an arguments,simba fans please try to fake your ID inorder to get acuracy informations,young africans is still young to simba but lets wait and see.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic